Nemesi wa Aleksandria

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Nemesi wa Aleksandria (alifariki 250 hivi) alikuwa Mkristo wa Misri aliyefia dini kwa kuchomwa moto katika mji huo wakati wa dhuluma ya kaisari Decius.

Kabla ya hapo aliwahi kufungwa kwa kusingiziwa kuwa mwizi, lakini mahakama ilithibitisha si kweli. Lakini dhuluma hiyo ilipoanza, alikamatwa tena na kushtakiwa mbele ya hakimu Emiliani kwamba ni Mkristo, na kwa amri yake aliteswa tena na tena na hatimaye kuhukumiwa achomwe moto pamoja na wezi, kwa mfano wa Yesu aliyesulubiwa pamoja na wahalifu wawili[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 10 Septemba[2] lakini pia 19 Desemba[3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads