Nihoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nihoni (Nihonium) ni elementi ya kikemia yenye alama Nh na namba atomia 113. Iliitwa pia eka-thallium. Haitokei kiasili maana ni elementi sintetiki inayoweza kutengenezwa katika maabara kutokana na mbunguo wa Moskovi.
Elementi hii ilitambuliwa mwaka 2004. Vikundi vya wanasayansi waliitafuta wakati uleule pale Dubna (Urusi) na Wako (Japani). Hatimaye Wajapani walikubaliwa kuwahi kutambua tabia zake nyingi wakachagua jina kufuatana na jina la kienyeji cha Japani, "Nihon". [1] , [2] , [3]
Nusumaisha ya Nihoni ni sekunde chache, kwa hiyo haikudumu muda wa kutosha kuangalia tabia zake; kila kiasi kinachotengenezwa kinapotea baada ya sekunde kadhaa. Hivyo hakuna matumizi kwa elementi hiyo yanayojulikana.
Kulingana na nafasi yake katika jedwali la elementi inawezekana ni metali laini yenye rangi ya fedha ikiwa na utendanaji mkali wa kikemia.
Remove ads
Marejeo
Tovuti za Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads