Moskovi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Moskovi (Moscovium) ni elementi sintetiki yenye alama Mc na namba atomia 115. Hali halisi haiko duniani isipokuwa kwa muda mfupi ikitengenezwa katika maabara. Iliundwa kwa mara ya kwanza mnamo 2003 na kundi la wanasayansi wa Urusi na Marekani waliofanya kazi pamoja kwenye Taasisi ya pamoja ya utafiti wa nyuklia (JINR) huko Dubna, Urusi.
Watafiti walifyatua ioni za Kalisi Ca-48 dhdi ya Ameriki Am-243 wakaunda atomu nne za Moskovi. Atomi hizu zilibungua katika muda wa milisekunde 100 kwa kutoa vyembe vya alpha hadi kuwa Nihoni. [1] [2]
Mwaka 2016, elementi hiyo mpya ilipewa jina rasmi kwa heshima ya Moscow Oblast, mkoa ambako JINR iko. [3]
Moskovi ni elementi nururifu sana; isotopi yake iliyo thabiti zaidi huwa na nusumaisha ya sekunde 0.65 pekee.[4]
Hakuna tabia za kifizikia au kikemia zilizoweza kutazamwa; hii ni kwa sababu ya uzalishaji mdogo na gharama kubwa [5] na ukweli kwamba hubungua haraka sana.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads