Oliver Plunkett

From Wikipedia, the free encyclopedia

Oliver Plunkett
Remove ads

Oliver Plunkett (kwa Kieire: Oilibhéar Pluincéid; Loughcrew, County Meath, Ireland, 1 Novemba 1625[1] – Tyburn, London, Uingereza, 1 Julai 1681) alikuwa askofu mkuu wa Armagh, kaskazini mwa Ireland, kuanzia mwaka 1670[2].

Thumb
Mt. Oliver alivyochorwa na Edward Luttrell.

Baada ya njama ya Kipapa aliendelea, ingawa kwa siri, kutokana na dhuluma ya serikali.

Hatimaye alikamatwa na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kueneza imani Katoliki[3]. Hivyo alinyongwa na kuraruliwa akisamehe wote na kukiri imani sahihi hadi mwisho.

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 23 Mei 1920, halafu Papa Paulo VI tarehe 12 Oktoba 1975 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads