Kizole

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kizole
Remove ads

Vizole ni ndege wadogo kiasi wa jenasi Onychognathus katika familia Sturnidae. Wanatokea Afrika tu isipokuwa kizole Somali na kizole Arabu ambao wanatokea nchi za kiarabu pia. Wanapenda kuwa kwa makundi. Ndege hawa wana mabawa mekundu yaonekanayo sana wakiruka anwani. Manyoya ya dume ni meusi na yale ya jike yana rangi ya kijivu cheusi. Hula wadudu na matunda hasa, lakini hula nusra kila kitu. Hulijenga tago lao juu ya kipande cha jabali kilichojitokeza nje katika mahali penye kulindwa. Kizole mabawa-mekundu hutaga mijini pia juu ya vishubaka au mahali pengine penye kulindwa. Jike huyataga mayai 2-4 buluu.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads