Oriensi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Oriensi (kwa Kifaransa: Orens; kwa Kilatini: Orientius; alifariki Auch, leo nchini Ufaransa, 450 hivi) alikuwa askofu wa mji huo na mshairi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei[1].

Maisha

Oriensi aliongoka baada ya kuishi katika dhambi akawa askofu mwenye sifa katika uchungaji wakati wa fujo zilizotokana na uhamaji wa makabila ya Kigermanik, akijitahidi kujenga amani kati yao na wenyeji, pamoja na kung'oa Upagani[2][3].

Alitunga utendi mrefu Commonitorium kuhusu maadili[4].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads