Pafnusi wa Tebe
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Pafnusi wa Tebe alikuwa mmonaki mfuasi wa Antoni Mkuu na wa Makari Mkuu, halafu askofu wa mji fulani wa Thebaid kaskazini (Misri) mwanzoni mwa karne ya 4.

Wataalamu wengine wanamhesabu kati ya wahusika muhimu wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325), alipotetea kwa nguvu zote imani sahihi, na wanasema aliongozana na Atanasi wa Aleksandria kushiriki Sinodi ya kwanza ya Turo (335).
Kabla ya hapo alidhulumiwa na serikali ya Dola la Roma akaharibiwa mguu wa kushoto na jicho la kulia kwa sababu ya imani yake akapelekwa kufanya kazi ya shokoa migodini wakati wa kaisari Galerius [1].
Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Aprili [2]; katika Kanisa la Kilatini tarehe 11 Septemba[3][4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo kwa Kiswahili
Marejeo mengine
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads