Pasiano

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pasiano
Remove ads

Pasiano (Hispania, 310 hivi - Barcelona, Hispania, 391 hivi) alikuwa askofu wa 2 wa mji huo kuanzia mwaka 365 hadi kifo chake.

Thumb
Mt. Pasiano kadiri ya Joan Roig na Joan Moxí.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa[1].

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Machi[2].

Maisha

Aliwahi kuoa na kuzaa mtoto aliyefanya kazi ikulu.

Jeromu alisifu maisha yake matakatifu pamoja na usafi wa moyo, ujuzi na ufasaha[3].

Katika kuhubiri alikuwa akisema jina lake ni Mkristo na ubini wake ni Mkatoliki[4][5].

Maandishi

Aliandika kuhusu mada mbalimbali, lakini vimetufikia kitabu kimoja juu ya toba na barua tatu tu[6].

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads