Patrick wa Ireland

From Wikipedia, the free encyclopedia

Patrick wa Ireland
Remove ads

Patrick wa Ireland (kwa Kilatini Patricius) aliishi kuanzia mwaka 387 hivi hadi tarehe 17 Machi 461[1] (wengine wanasema 493[2]).

Thumb
Mt. Patrick katika kioo cha rangi.
Thumb
Mahali panapodhaniwa kuwa alifanyiwa mazishi huko Downpatrick.

Ni maarufu kama Mkristo kutoka Uingereza aliyepata kuwa mmisionari mkuu wa Ireland na anaheshimiwa kama mtakatifu msimamizi wa kisiwa hicho [3].

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifo chake[4].

Remove ads

Maisha

Kati ya maandishi yake, zimetufikia barua mbili, ambamo tunapata habari za kuaminika juu yake, tofauti na nyingine nyingi ambazo zinatia shaka.[5]

Alipokuwa na umri wa miaka 16 hivi huko Wales, alitekwa na maharamia kutoka Ireland na kufanywa mtumwa kisiwani huko.

Baada ya miaka 6 alifaulu kukimbia na kurudi kwenye familia yake.

Lakini akajisikia wito wa kuinjilisha wakazi wa kisiwa hicho, hivyo baada ya kujiandaa katika monasteri ya Ufaransa akarudi huko kama askofu akafanya kazi hasa kaskazini na magharibi akitangaza kwa bidii Injili kwa wote na kuongoza kwa nguvu Kanisa lake.[6][7]

Remove ads

Sala yake

Kristo uwe nami, Kristo uwe ndani mwangu,

Kristo nyuma yangu, Kristo mbele yangu,

Kristo karibu nami, Kristo ili unitawale,

Kristo, ili unifariji na kunifundisha,

Kristo pamoja nami, Kristo juu yangu,

Kristo katika amani, Kristo katika hatari,

Kristo moyoni mwa wote wanaonipenda,

Kristo mdomoni mwa rafiki na mgeni.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads