Paulo Ho Hyob
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paulo Ho Hyob (1796 - Seoul, 30 Januari 1840) ni mmojawapo katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Askari, alikamatwa na kuteswa kwa kukiri imani ya Kikristo. Alipozidiwa, alionekana kutaka kushindwa, kumbe akatubu na kuthibitisha mara imani yake mbele ya hakimu; kwa ajili hiyo, baada ya kufungwa muda mrefu, alikufa kwa mateso yaliyompata [1].
Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, ila ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads