Paulo Nguyen Van My

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Paulo Nguyen Van My (1798 - 1838) alikuwa katekista wa Vietnam ambaye alidumu imara katika imani ya Kikristo hata akanyongwa pamoja na wenzake Petro Truong Van Dong na Petro Vu Van Truat katika dhuluma ya kaisari Minh Mang [1].

Ni kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 18 Desemba[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads