Peloponesi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Peloponesi
Remove ads

Peloponesi (Kigiriki Πελοπόννησος peloponesos) ni rasi ya kusini mwa Ugiriki. Imeunganika na sehemu ya bara ya nchi kwa shingo la nchi kwenye mji wa Korintho.

Thumb
Peloponesi katika Ugiriki

Jina la kihistoria la rasi lilikuwa Morea (Μωριάς morias).

Eneo lote la Peloponesi ni kilomita za mraba 21,549. Kuna watu 1,155,000 walioishi huko mwaka 2011.

Peninsula imegawanywa kati ya mikoa mitatu ya kiutawala: sehemu kubwa ni ya mkoa wa Peloponesi, na sehemu ndogo ni za mkoa wa Ugiriki Magharibi na wa Attica.

Remove ads

Jiografia

Thumb
Shingo la nchi la Korintho, mji wa Korintho ukiwa upande wa kushoto, mstari nyoofu wa Mfereji wa Korintho katikati ya picha

Ghuba ya Korintho inatenganisha Peloponesi na Ugiriki bara.

Rasi hiyo ina milima mingi na pwani yenye hori ndefu zinazoingia ndani ya nchi. Mlima mrefu ni Taygetos unaofikia mita 2,407 juu ya UB. Rasi yote inakabiliwa na mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.

Mji mkubwa zaidi ni Patras yenye wakazi 170,000.

Miji

Miji mikubwa zaidi ya kisasa kwenye Peloponesi ni (sensa ya 2011):

  • Patras - wenyeji 170,896
  • Kalamata - wenyeji 62,409
  • Korintho - wenyeji 38,132
  • Tripoli - wenyeji 30,912
  • Aigio - wenyeji 26,523
  • Pyrgos - wenyeji 25,180
  • Argos - wenyeji 24,700
  • Sparta - wenyeji 19,854
  • Nafplio - wenyeji 18,910
Remove ads

Historia

Thumb
Lango la Simba huko Mikene (Mycenae).
Thumb
Hekalu la Hera, Olimpia.

Rasi hii iliona vipindi na watendaji muhimu katika historia ya Ugiriki ya Kale.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads