Peramiho
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Peramiho ni kata ya Wilaya ya Songea Vijijini katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania, yenye postikodi namba 57213.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,503 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,031 waishio humo. [2].
Remove ads
Abasia na parokia
Inajulikana hasa kutokana na abasia ya wamonaki Wakatoliki Wabenedikto.
Abasia hiyo ilianzishwa kama kituo cha umisionari na P. Cassian Spiess O.S.B. aliyefika Peramiho mwaka 1898.
Mnamo mwaka 1931 Peramiho ilifanywa kuwa abasia na pia makao ya jimbo chini ya Abate-Askofu Gallus Steiger O.S.B..
Makao ya jimbo yalihamishiwa Songea mnamo mwaka 1969, na siku hizi kuna majimbo matatu (Jimbo kuu la Songea, Jimbo Katoliki la Njombe na Jimbo Katoliki la Mbinga) yaliyotokana na jimbo la zamani la Peramiho.
Peramiho kuna shule na hospitali nzuri pamoja na monasteri.
Pia ni makao makuu ya parokia ya Peramiho ambayo ina vigango vifuatavyo: Parangu, Lilambo, Likuyu, Mwanamonga, Litowa, Nakahuga, Sinai, Maposeni, Mdunduwalo na Morogoro.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads