Petro Khanh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Petro Khanh (1780-1842) alikuwa padri wa Vietnam ambaye, kisha kutambulika kama Mkristo kwenye ofisi ya kodi, alifungwa miezi sita ambapo alikataa daima kuasi imani yake, na hatimaye alikatwa kichwa kwa amri ya kaisari Thieu Tri [1].
Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 12 Julai[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads