Petro Yi Hoyong
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Petro Yi Hoyong (Icheon, 1803 - Seoul, 25 Novemba 1838) alikuwa katekista wa Korea aliyekamatwa na askari akiwa pamoja na dada yake, Agata Yi Sosa.
Katika dhuluma alibaki imara katika kuungama imani yake, ingawa walimvunja mifupa mara tatu na kumuacha gerezani miaka 4, hadi alipofariki dunia[1].
Ni wa kwanza katika kundi kubwa la Wakristo wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa kwa ajili ya imani yao katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000.
Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[2]
Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 25 Novemba[3].
Remove ads
Mazingira
Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[4] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[5].
Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads