Pierio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Pierio (alifariki Roma baada ya mwaka 309)) alikuwa padri wa Misri ambaye inawezekana alikuwa mkuu wa Chuo cha Aleksandria kabla ya Achilas wa Aleksandria.
Mwanafalsafa maarufu, lakini maarufu zaidi kwa uadilifu na ufukara wa hiari, alifundisha waumini kwa bidii kuhusu Biblia ya Kikristo wakati Theonas alikuwa patriarki wa Alexandria[1]
Baada ya Mateso ya Wakristo kwisha, alihamia Roma alipofariki [2].
Sehemu chache tu za maandishi yake zimetufikia[3][4][5][6].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, ingawa si rahisi kwamba alifia dini yake walivyosema Fosyo na wengine[7].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Novemba[8] au 29 Novemba.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads