Plinio Mzee

From Wikipedia, the free encyclopedia

Plinio Mzee
Remove ads

Gaius Plinius Secundus (anafahamika zaidi kama Plinio Mzee; 23 BK - 25 Agosti 79 BK) alikuwa mwandishi na mwanafalsafa wa utamaduni wa Roma ya Kale, aliyewahi kuwa pia kiongozi wa kijeshi na rafiki wa karibu wa Kaizari Vespasian .

Thumb
Plinio Mzee, jinsi msanii Mfaransa alivyomwaza katika karne ya 19.
Ukweli wa haraka Plino Mzee au Gaius Plinius Secundus, Makazi ...

Akitumia wakati wake mwingi kusoma, kuandika au kuchunguza hali ya asili na jiografia, aliandika kitabu kirefu cha Historia Asilia ("Naturalis Historia"), ambacho kilikuwa mfano kwa waandishi wengi waliomfuata.

Plinio Mzee alikufa mnamo 25 Agosti mwaka 79 KK alipotaka kuokoa marafiki waliojaribu kukimbia kutoka mlipuko wa Mlima Vesuvio; volkeno hiyo iliteketeza miji ya Pompeii na Herkulaneo.

Remove ads

Historia Asilia ya Plinio

Historia Naturalis ni kati ya kazi kubwa za utaalamu zilizodumu kutoka zamani za Roma ya Kale hadi leo. Plinio alilenga kukusanya elimu yote iliyopatikana wakati wake. Alidai mwenyewe kuwa Mroma wa kwanza aliyefanya kazi kubwa ya aina hiyo, akikusanya habari za botania (elimu ya mimea), zoolojia (elimu ya wanyama), astronomia (elimu ya nyota), jiolojia na elimu madini pamoja na matumizi ya rasilimali hizo.

Maelezo yake kuhusu teknolojia mbalimbali ni chanzo cha pekee kwa elimu yetu siku hizi kuhusu njia zilizotumiwa zamani kuchimba madini, kujenga majengo makubwa au kusaga nafaka. Sehemu ya maandishi yake ziliweza kuthibishwa na uchunguzi wa akiolojia. Maandiko hayo ni chanzo cha pekee kinachoeleza kazi ya wasanii wa siku zile, hivyo ni marejeo kwa historia ya sanaa.

Historia Naturalis imekuwa kielelezo kwa mfumo wa kamusi elezo za baadaye kwa kuzingatia upana wa mada, kuonyesha vyanzo vya habari na kutaja kazi za waandishi waliotangulia, hatimaye katika kupanga orodha ya yaliyomo yake.

Kazi imejitolea Mfalme Tito, mwana wa rafiki Pliny ya karibu, Mfalme Vespasian, katika mwaka wa kwanza wa Titus 'utawala. Ni kazi pekee ya Pliny kunusurika, na ya mwisho aliyoichapisha, ikikosa marekebisho ya mwisho wakati wa kifo chake cha ghafla na kisichotarajiwa katika mlipuko wa Vesuvius wa AD 79. Alitoa kazi hiyo kwa heshima ya Kaizari Tito aliyekuwa mtoto wa kwanza na mrithi wa rafiki ya Vespansiano.

Kazi yote ya Historia Asilia imegawiwa kwa vitabu 37:

1 Dibaji na orodha ya yaliyomo, orodha ya marejeo
2 Maelezo ya kihisabati na kimaumbile ya ulimwengu
3 - 6 Jiografia na ethnografia
7 Anthropolojia na fiziolojia ya binadamu
8 – 11 Zoolojia
12 – 27 Botania, pamoja na kilimo, elimu ya bustani na elimu ya madawa
28 – 32 Elimu ya madawa
XXXIII – XXXVII Uchimbaji madini na madini, haswa katika matumizi yake kwa maisha na sanaa, pamoja na:
dhahabu
kukalibu fedha [1]
sanamu za shaba [2]
uchoraji [3]
uchongaji [4]
sanamu za marumaru [5]
mawe ya thamani na vito [6]
Remove ads

Marejeo

Vyanzo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads