Prokopi Mkuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Prokopi Mkuu (Yerusalemu, Palestina, karne ya 3 - Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 8 Julai 303) alikuwa Mkristo aliyeuawa kwa kukatwa kichwa katika mji huo mara alipoanza kutetea kwa ushujaa imani yake mahakamani mwanzoni mwa dhuluma ya kaisari Diokletian[1].

Kabla ya hapo aliishi kwa uadilifu na wema[2], pamoja na kuwa mtaalamu wa falsafa na teolojia[3][4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Julai[5] au 22 Novemba[3][4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads