Ray C.

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia

Ray C.
Remove ads

Rehema Chalamila (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Ray C; amezaliwa Iringa, Tanzania, 15 Mei 1982) ni mwimbaji wa muziki wa R&B, dansi, na bongo-bhangra kutoka nchini Tanzania.

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Remove ads

Wasifu

Kabla ya kujihusisha na muziki, Ray C aliwahi kufanya kazi kama mtangazaji wa redio ya East Africa kabla ya kwenda redio ya Clouds FM ya jijini Dar es Salaam.

Mnamo mwaka 2003 alitoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Mapenzi Yangu".

Alianza kujulikana baada ya kutoa vibao kadhaa kama vile; Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Nawewe Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu kama mwimbaji aliyeutingisha muziki wa Bongo Flava kati ya 2003-2009 — hadi hapo alipokuja kuingia matatani kiafya baada ya kutumia dawa za kulevya.

Mwaka wa 2012, Rais wa Tanzania wakati huo, Jakaya Kikwete, alitoa msaada mkubwa wa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ray C na baada ya huduma mwimbaji huyu alikwenda kumshukuru kwa msaada wake.[1]

Mwaka wa 2016 imeripotiwa ya kwamba Ray C amerudi tabia yake ya kutumia dawa za kulevya, hali ambayo ilimkera sana Kikwete.

Remove ads

Muziki

Albamu:

  • Mapenzi Yangu (2003)
  • Na Wewe Milele (2004)
  • Sogea Sogea (2006)
  • Touch Me (2008)

Tuzo

Mshindi:

  • 2004 Tanzania Music Awards - Msanii Bora wa kike [2]
  • 2004 Kisima Music Awards - Msanii wa kike kutoka Uganda & Tanzania
  • 2007 Tanzania Music Awards - Msanii Bora wa kike [3]

Mshiriki:

  • 2006 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania)[4]
  • 2005 Channel O Music Awards - Msanii bora Afrika ya Mashariki
  • 2007 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania)
  • 2008 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania) [5]
  • 2011 Tanzania Music Awards - Video bora, Wimbo bora, Wimbo bora wa Afro Pop and Wimbo bora wa kushirikishwa ('Mama Ntilie' with Gelly wa Ryme & AT)[6]

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads