Regina caeli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Regina caeli
Remove ads

"Regina caeli" (tamka: reˈdʒina ˈtʃeli; maana yake Malkia wa Mbingu)ni antifona inayotumika kumuelekea Bikira Maria katika Kanisa la Kilatini wakati wa Pasaka, kuanzia Dominika ya Ufufuko wa Yesu hadi Pentekoste.

Antifona ikiimbwa.
Thumb
Nota za Regina caeli[1]

Katika siku hizo hamsini ndiyo antifona pekee inayotumika kumalizia Sala ya mwisho ya Liturujia ya Vipindi [2] lakini pia inashika nafasi ya sala ya Angelus (inayofanyika mara tatu kwa siku: asubuhi, adhuhuri na jioni).

Remove ads

Maneno asili kwa Kilatini

  • Regina caeli, laetare, alleluia;
  • Quia quem meruisti portare, alleluia,
  • Resurrexit, sicut dixit, alleluia:
  • Ora pro nobis Deum, alleluia.[3]

Tafsiri ya Kiswahili

  • Malkia wa mbingu, furahi, aleluya;
  • Kwani uliyestahili kumchukua, aleluya,
  • Amefufuka, alivyosema, aleluya:
  • Utuombee kwa Mungu, aleluya.[4]

Historia

Mtunzi wa Regina caeli hajulikani. Kimaandishi inapatikana katika kitabu cha antifona cha mwaka 1200 hivi kinachotunzwa katika Basilika la Mt. Petro, huko Vatikani, jijini Roma.[5]

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads