Mikoa ya Mali

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mikoa ya Mali
Remove ads

Mikoa ya Mali ni magatuzi ya nchi ya Mali kwenye ngazi ya juu. Tangu mwaka 2016 Mali imegawanywa katika mikoa kumi na eneo la pekee la mji mkuu.

Thumb
Ramani ya Mali (ugawaji kabla ya mwaka 2016)

Mnamo mwaka 2012 sheria ilitangaza kugawiwa upya kwa nchi katika mikoa 19 kutoka ile 8 ya awali[1]. Hadi mwaka 2021 kuna mikoa miwili mipya pekee iliyoanzishwa, ambayo ni Taoudenit (iliyomegwa kutoka Mkoa wa Timbuktu) na Menaka (zamani kwenye Mkoa wa Gao).[2] [3]

Kila mkoa unaitwa jina la mji mkuu wake. Mikoa imegawanywa katika wilaya (cercles) 56. Wilaya zote zimegawanywa katika manispaa (communes) 703. [4]

Remove ads

Jiografia

Mikoa 5 ni hasa jangwa, na mikoa hiyo ina nusu ya eneo lote la nchi.

Mkoa mkubwa zaidi ni Taoudenit, mdogo zaidi ni Segou.

Demografia

Mkoa wenye watu wengi zaidi ni Sikasso wenye watu milioni 2.6, na ule wenye watu wachache zaidi una watu 68,000 pekee.

Mikoa

Mikoa imepewa namba kwa kutumia namba za Kiroma.[5] Mji mkuu wa Bamako unasimamiwa kama eneo la pekee.

Mikoa kumi na eneo la Bamako vimeorodheshwa hapa chini. Idadi ya wakazi ni kutokana na sensa za 1998 na 2009. [6]

Thumb
Mikoa ya Mali (mnamo 2016)
Maelezo zaidi Jina la mkoa, Nambari ya mkoa ...

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads