Reuters

shirika la habari la kimataifa From Wikipedia, the free encyclopedia

Reuters
Remove ads

Reuters ni shirika la habari linalomilikiwa na Thomas Reuters[1] Ni kati ya vyombo vya habari vikubwa na vinavyoaminiwa sana ulimwenguni ingawa lina mwelekeo wake kisiasa.

Thumb
Reuters London
Thumb
Nembo ya Reuters (imetolewa 2020)

Shirika hili limeajiri waandishi wa habari takriban 2500 na wapiga picha habari wapatao 600 waliosambazwa kwenye vituo 200 katika maeneo mbalimbali ya dunia na kuripoti katika lugha 16 tofauti.

Shirika hili liliasisiwa jijini London mnamo mwaka 1851 na mtu mwenye asili ya Ujerumani, Paul Reuters. Baadaye lilinunuliwa na Thomson Corporation ya Canada mnamo mwaka 2008 na sasa limekuwa tawi linaloshughulika na habari la kampuni kuu ya Thomson Reuters.[2]

Remove ads

Historia

Karne ya 19

Thumb
Paul Reuter, mwasisi wa Reuters (picha iliyopigwa na Nadar, mwaka 1865)

Paul Reuter alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya uchapishaji wa vitabu ya mjini Berlin na alijihusisha na usambazaji wa majarida ya watu wenye misimamo mikali nyakati za mwanzoni mwa "Mapinduzi ya Machipuko ya Mataifa ya Mwaka 1848" (The 1848 Springtime of Nations Revolutions). Machapisho hayo yalimfanya Reuters kufikiri sana, na mnamo mwaka 1850 akaanzisha shirika lake la habari kama majaribio huko Aachen akitumia utaratibu wa usambazaji wa nyumba kwa nyumba na telegramu kuanzia 1851 na kuendelea, ili kutuma arafa baina ya Brussels na Aachen,[3] kwenye mtaa ambao leo una Jumba la Reuters la Aachen.

Reuter alihamia London mnamo mwaka 1851 na kuanzisha kampuni ya uwakala wa habari kwenye eneo lililojulikana kama The London Royal Exchange. Ikiwa na makao yake makuu jijini London, kampuni ya Reuter ilianza na kujishughulisha na habari za biashara, benki za akiba, mashirika ya udalali (brokerage houses) na wabia wa kibiashara.[4] Mteja wake wa kwanza kujisajili lilikuwa gazeti la Morning Advertiser la London mnamo 1858, na muda mfupi baadae wengine wengi walijiunga.[4][5] Kwa mujibu wa Encyclopædia Britannica: "thamani ya Reuters kwa magazeti haikutokana tu na habari za biashara ilizowapa Bali kutokana na uwezo wake wa kuwa wa kwanza kuripoti stori zenye umuhimu wa kimataifa."[4] Kwa mfano, Reuters ilikuwa ya kwanza kuripoti Ulaya juu ya kuuwawa kwa Abraham Lincoln mnamo 1865.[4][6]

Mnamo mwaka 1865, Reuter aliibadili kampuni yake binafsi kuwa kampuni ya washirika na kuitwa Reuter's Telegram Company Limited; Reuter akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni.[7]

Mwaka 1870 Shirika la Habari la Ufaransa Havas (lililoanzishwa mwaka 1835), Shirika la Uingereza la Reuters (lililoanzishwa 1851) na shirika la Wolff la Ujerumani (lilianzishwa 1849) yalisainiana mkataba (uliojulikana kama The Ring Combination) ambao ulikuwa wa kugawana himaya za kibiashara kati yao. Kila shirika lilifanya mikataba yake kivyake na mashirika mengine ya nchini mwake na yaliyo kwenye nchi za kwenye himaya yake. Kiuhalisia, Reuters, ambao ndio waliobuni wazo, walionekana kuutawala muungano huo. Ushawishi wake ulikuwa mkubwa zaidi kwani eneo ililotawala lilikuwa kubwa na lenye kutoa habari muhimu zaidi kuliko yale mengine. Pia, Reuters walikuwa na wafanyakazi wengi zaidi pamoja na wawakilishi na waandishi madei-waka duniani kote na hivyo wao ndio walioleta dimbani habari nyingi zaidi asilia. Udhibiti wa Uingereza wa njia za simu uliifanya London yenyewe kuwa kitovu cha habari za ulimwengu cha kupigiwa mfano, hali iliyoimarishwa zaidi na shughuli lukuki na za aina mbalimbali za kibiashara, masoko ya fedha na mitaji na zile za dola la kifalme.[8]

Mwaka 1872, Reuter's ilijitanua hadi Mashariki ya Mbali, ikafuatiwa na Amerika ya Kusini mnamo 1874. Katika awamu zote za utanukaji, kiwezeshi kikubwa kilikuwa ni teknolojia ya juu ya utumaji habari kwa njia za juu ya ardhi na zile za chini ya bahari.[6] Mnamo 1878, Reuter alistaafu nafasi yake ya ukurugenzi mkuu, na kurithiwa na mwanawe mkubwa, Herbert de Reuter.[7] Mnamo 1883, Reuter's ilianza kutuma habari kupitia mawimbi ya umeme kwenda kwa magazeti ya London.[6]

Karne ya 20

Thumb
Roderick Jones, meneja mkuu 1915–1941

Mtoto wa Reuter, Herbert de Reuter, aliendeleza kazi ya umeneja mkuu mpaka alipopatwa na umauti kwa kujiua mnamo mwaka 1915. Kampuni ikarudi kwenye mfumo wa umiliki binafsi mnamo mwaka 1916, ambapo hisa zote zilinunuliwa na Roderick Jones (1877–1962) na Mark Napier; wakabadilisha jina la kampuni na kuwa "Reuters Limited", wakiondoa alama ya kiuandishi ya kimilikishi (').[7] Mnamo mwaka 1919, ripoti kadhaa za Reuters zilieneza uongo juu ya maandamano ya kupinga ukoloni ya Korea Kusini kwa kuyaita machafuko mabaya ya kupinga Vuguvugu la Bolshevik. Watafiti wa Korea Kusini walibaini kuwa sehemu kubwa ya ripoti hizo zilinukuliwa kwenye magazeti mbalimbali ya kimataifa na kuathiri mtazamo wa dunia juu ya nchi hiyo.[9] Mnamo mwaka 1923, Reuters ilianza kutumia redio kutangaza habari ulimwenguni, na kuwa ndio mwanzilishi.[6] Mnamo 1925, the Press Association (PA) la Uingereza lilinunua na kuhodhi sehemu kubwa ya hisa za Reuters, na kufikia umiliki kamili miaka michache baadae.[4] Katika vipindi vya vita vikuu vya dunia, gazeti la The Guardian liliripoti kuwa Reuters ilishinikizwa na serikali ya Uingereza ifanye kazi kwa maslahi ya taifa. Mnamo 1941, Reuters ilikwepa shinikizo hilo kwa kubadili muundo wake na kuwa kampuni binafsi."[6] Mnamo mwaka 1941, the PA ikaiuza nusu ya Reuters kwa the Newspaper Proprietors' Association, na hali hiyo ya umiliki wa pamoja ilitanuliwa mnamo mwaka 1947 kwa kuzihusisha na jumuia zinazowakilisha magazeti ya kila siku huko New Zealand na Australia.[4] Wamiliki wapya wakaanzisha Kabidhi Wasihi wa Reuters. Kanuni za Kabidhi Wasihi wa Reuters ziliwekwa ili kulinda uhuru wa kampuni.[10] Katika hatua hiyo, Reuters ilitokea kuwa moja ya mashirika makubwa ya habari ulimwenguni, ikisambaza habari kwa magazeti na mashirika mengine ya habari, kadhalika kwa warusha matangazo ya redio na televisheni."[4] Hali kadhalika, katika hatua hiyo, Reuters ilikuwa "msambazaji mkuu wa habari kwa vyombo vikuu karibu vyote duniani na kwa maelfu ya vyombo vingine vilivyo vidogo vidogo, ama moja kwa moja au kupitia wakala wa habari wa nchi hizo," hiyo ni kwa mujibu wa Britannica.[4]

Mwaka 1961, Reuters ilinyakua habari za usimamishaji wa Ukuta wa Berlin na kuzitangaza.[11] Reuters ikawa miongoni mwa mashirika ya kwanza kutuma habari za kibiashara zilizo kwenye kompyuta kupitia njia (mkongo) za baharini miaka ya 1960.[4] Mnamo 1973, Reuters "ilianza kuonesha taarifa za kima cha ubadilishaji fedha moja kwa moja kwenye skrini za kompyuta za wateja wake kule walikokuwa."[4] Mnamo 1981, Reuters ilianza kuwezesha ufanyikaji wa miamala ya kielektroniki kwenye mtandao wake wa kompyuta kisha ikatengeneza mifumo kadhaa ya udalali wa kielektroniki na huduma nyingine za kibiashara za kielektroniki.[4] Reuters ikarejea tena kuwa kampuni inayomilikiwa na wengi mnamo mwaka 1984,[11] wakati Kabidhi Wasihi yake ilipoorodheshwa kwenye masoko ya fedha[6] kama vile London Stock Exchange (LSE) na NASDAQ.[4] Baadae, Reuters ilikuwa ya kwanza kuchapisha habari za kutaka kuangushwa kwa ukuta wa Berlin mnamo 1989.[11]

Reuters ndiyo iliyokuwa ikiongoza katika tasnia ya habari mtandaoni katika miaka ya tisini. Ilipata hadhi hiyo kwa kuingia ubia na ClariNet pia PointCast, ambao walikuwa waanzilishi wa mwanzo wa utoaji habari mtandaoni.[12]

Karne ya 21

Bei ya hisa za Reuters ilipanda kwenye kipindi cha dotcom boom (Kipindi cha kibiashara na uchumi ambacho kilitoa matumaini makubwa ya kushamiri na kupatikana kwa faida kubwa za biashara kupitia mtandao na kuvutia uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya kimtandao), kisha ilianguka kufuatia kipindi cha matatizo ya mabenki cha 2001.[6] Mnamo 2002, Britannica iliandika kwamba sehemu kubwa ya habari ulimwenguni kote zilijiri kupitia mashirika makubwa matatu: the Associated Press, Reuters, na Agence France-Presse.[13]

Kufikia 2008, shirika la habari la Reuters lilikuwa ni sehemu ya kampuni kuu inayojitegemea ya Reuters Group plc. Reuters ikanunuliwa na Thomson Corporation ya Canada mnamo 2008, na kuunda Thomson Reuters.[4] Mnamo 2009, Thomson Reuters ilijiondoa kwenye masoko ya hisa ya LSE na NASDAQ, badala yake ikaorodhesha hisa zake kwenye masoko ya Toronto Stock Exchange (TSX) na na Soko la hisa la NewYork (New York Stock Exchange (NYSE)).[4] Mwanzilishi wa Reuters aliyekuwa amebaki Marguerite, Baroness de Reuter, alifariki akiwa na umri wa miaka 96 tarehe 25 January 2009.[14] Kampuni mama ya Thomson Reuters ina makao yake makuu jijini Toronto, na hutoa huduma za taarifa za kifedha kwa wateja wake na wakati huohuo ikiendesha shughuli zake za kawaida za wakala wa habari.[4]

Mnamo 2012, Thomson Reuters ilimteua Jim Smith kuwa Mkurugenzi wake Mkuu.[10] July 2016, Thomson Reuters ilifikia makubaliano ya kuuza hati miliki zake za vitu vya ubunifu na miradi ya kisayansi Kwa kiasi cha dola bilioni 3.55 kwa makampuni ya kibinafsi ya ukuzaji ufanisi (private equity firms).[15] Mnamo Oktoba 2016, Thomson Reuters ilitangaza mipango yake wa upanuzi kibiashara na kuhamia Toronto.[15] Ikiwa ni sehemu ya mpango wa kupunguza gharama na kujisuka upya, mwezi Novemba 2016, Thomson Reuters Corp. ilizifuta nafasi za kazi 2,000 kwenye maeneo mbalimbali duniani kati ya ajira zake takriban 50,000.[15] Tarehe 15 Machi 2020, Steve Hasker aliteuliwa kuwa rais na Mkurugenzi Mkuu.[16]

Mwezi Aprili 2021, Reuters ilitangaza kuwa tovuti yake itakuwa ikipatikana kwa kulipiwa, hatua waliyoifikia kufuatia wapinzani wake kufanya hivyo.[17][18]

Mwezi Machi 2024, Gannett, mchapishaji mkubwa wa magazeti nchini Marekani, ilisaini mkataba na Reuters ili itumie maudhui ya Reuters yapitiayo kwenye mtandao habari wake wa hadhi ya kiulimwengu ikiwa ni kufuatia kuvunjika kwa mkataba wake na shirika la Associated Press.[19]

Mnamo 2024 hiyo hiyo, wafanyakazi wa Reuters walishinda Tuzo ya Uhabarishaji wa Kitaifa ya Pulitzer kupitia kazi zao juu ya utovu wa kiutendaji kwenye makampuni ya Elon Musk, ikijumuisha SpaceX, Tesla, and Neuralink, Hali kadhalika Tuzo ya Pulitzer kuhusu Upigaji Picha Unaoambatana na Habari za Hivi Punde zilizoangazia Vita vya Israeli na Hamas .[20]

Remove ads

Kuuwawa kwa waandishi

Reuters imeajiri waandishi wa habari takriban 2500 na wapiga picha habari wapatao 600 ambao wamesambazwa katika maeneo mbalimbali duniani yapatayo 200[21]. Lakini, kwa miaka, wamekuwa wakipatwa na madhila mbalimbali ikiwemo kupoteza maisha wakiwa kwenye kazi zao (jedwali linalofuata);

Waliokufa kwenye majukumu

Maelezo zaidi Jina, Utaifa ...
Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads