Roderiko Aguilar
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Roderiko Aguilar (kwa Kihispania Rodrigo Aguilar Alemán, Sayula, 13 Mei 1875 - Ejutla, Jalisco, Mexico, 28 Oktoba 1927) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Meksiko hadi alipouawa bila kesi kwa kutundikwa na askari mtini wakati wa Vita vya Wakristero. Hivyo alijaliwa kufia dini yake kama alivyotamani sana [1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Novemba 1992 halafu mtakatifu mfiadini tarehe 21 Mei 2000 pamoja na wenzake 24 waliofia dini katika vita hivyo[2]:
Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 21 Mei ila ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads