Rosh Hashanah
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rosh Hashanah (kwa Kiebrania: רֹאשׁ הַשָּׁנָה, Rōʾš hašŠānā, yaani "mwanzo wa mwaka") ni siku ya kwanza ya mwaka wa Kiyahudi. Ni sikukuu ya kwanza katika mfuatano wa siku takatifu za Uyahudi kwenye mwanzo wa mwaka jinsi zilivyobainishwa na Mambo ya Walawi 23:23–25 [1]. Tarehe yake hutokea kwa kawaida katika mwezi wa Septemba, hadi 5 Oktoba.

Rosh Hashanah ni maadhimisho na sherehe ya siku mbili ambayo huanza siku ya kwanza ya mwezi wa Tishri, ambao ni mwezi wa saba baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Hukumbuka uumbaji wa Adamu na Hawa waliokuwa watu wa kwanza kufuatana na taarifa ya Biblia.
Remove ads
Jina
Rosh ni neno la Kiebrania kwa "kichwa", ha ni kibainishi (kama "the" ya Kiingereza), na shana inamaanisha "mwaka". Hivyo Rosh HaShanah inamaanisha "mwanzo wa mwaka" na hivyo ni sikukuu ya Kiyahudi ya Mwaka Mpya.[2][3]
Rosh Hashanah inaashiria mwanzo wa mwaka mpya katika kalenda ya Kiebrania ambapo mwaka unapokea jina jipya. Huu ni mwaka wa kiraia, tofauti na miaka mingine inayopatikana ndani ya kalenda ya Kiyahudi. Mwaka wa kiraia ni tofauti na mwaka wa kidini unaoamulia tarehe za sikukuu. Hii ni pia sababu kwamba mwezi Tishri ambamo Rosh Hashana ni tarehe ya kwanza huitwa "mwezi wa saba". [4] Ni mwaka mpya kwa watu, wanyama, na mikataba ya kisheria.
Rosh Hashanah inaadhimisha uumbaji wa watu. [5]

Remove ads
Desturi za Sikukuu
Desturi za Rosh Hashanah ni pamoja na kupiga shofar (pembe ya kondoo dume iliyosafishwa), kama ilivyoagizwa katika Torati, kufuatia maagizo ya Biblia ya Kiebrania ya "kupiga baragumu" kwenye Yom Teruah[6] . Desturi zake ni pamoja na kuhudhuria ibada ya sinagogi, pamoja na kufurahia milo ya sikukuu; kwa mfano tufaha zilizowekwa kwenye asali, kutarajia kuamsha mwaka mpya mtamu.
Tarehe
Tarehe ya Rosh Hashanah inacheza kwa mujibu wa Kalenda ya Gregori kwa sababu miezi ya Kiyahudi inalingana na mwonekano wa Mwezi angani.
Rosh Hashanah hutokea siku 163 baada ya siku ya kwanza ya Pasaka, na hivyo kwa kawaida (lakini si mara zote) huamuliwa na mwezi mpya ulio karibu zaidi na ikwinoksi ya Septemba.
Kwa mujibu wa kalenda ya Gregori, tarehe ya kwanza kabisa ambapo Rosh Hashanah inaweza kutokea ni 5 Septemba, kama ilivyotokea mwaka wa 1842, 1861, 1899, na 2013. Tarehe ya mwisho ambapo Rosh Hashanah inaweza kutokea ni 5 Oktoba, kama ilivyotokea mwaka wa 1815, 1929, na 1967, na itatokea tena mwaka wa 2043.
Baada ya mwaka 2089, tofauti kati ya kalenda ya Kiyahudi na kalenda ya Gregori itasababisha Rosh Hashanah kutokea si mapema zaidi ya 6 Septemba. Kuanzia 2214, tarehe mpya ya mwisho itakuwa 6 Oktoba. [7]
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads