Rudewa
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rudewa ni kata ya Wilaya ya Kilosa katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67411.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 26,169 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,352 [2] waishio humo.
Kilimo cha mpunga na mahindi ni kati ya vitu ambavyo wananchi wanavitegemea pamoja na kiwanda cha mkonge kilichopo Rudewa Kambini.
Ina shule za msingi kama Rudewa Batini, Rudewa Mbuyuni, Rudewa Peapea, Unone na Rudewa Gongoni. Pia ina shule ya sekondari ya Rudewa.
Kata hii ina mabonde na mito isiyokauka kama mto Wami.
Wafugaji pia wanapatikana kama Wamasai na Wasukuma, mbali ya makabila kama Waha, Wamakua, Wamatumbi na Wazigua.
Ina vijiji kama Peapea, Mbuyuni, Rudewa, Gongoni na Unone.
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads