Rufo wa Roma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Rufo wa Roma (alifariki Roma, Italia, karne ya 1) alikuwa kati ya Wakristo wa kwanza wa jiji hilo.

Mtume Paulo katika Waraka kwa Warumi anamuita mteule wa Bwana akimsalimu pamoja na mama yake (Rom 16:13). Inawezekana alikuwa mtoto wa Simoni wa Kurene (Mk 15:21) [1][2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Novemba[4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads