Ruiru
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ruiru ni mji wa Kaunti ya Kiambu, ipatikanayo katikati ya Kenya.
Jiografia
Mji huu uko katika umbali wa takribani kilomita 3 kutoka katika Mpaka wa Nairobi.
Una eneo la km2 292 na umezungukwa na mashamba ya Kahawa. Ruiru ni mmoja kati ya miji inayotambulika zaidi nchini Kenya, ambao unaweza kufikika kwa urahisi kupitia barabara au reli.
Idadi ya Wakazi
Mji huu umekuwa na ongezeko la idadi ya watu, kutokana na uhaba wa nyumba mjini Nairobi.
Mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 238,858[1].
Hata hivyo, mji huu umeng'ang'ana kuwatosheleza wakazi wake.
Uchumi

Wengi wa wakazi wa Ruiru ni wafanyabiashara wenye asili ya Kikuyu.
Mji huu pia una matawi ya benki kadhaa kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays.
Pia kuna viwanda mbalimbali katika mji huo.
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads