Rujewa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Rujewa ni kata ya Wilaya ya Mbarali katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 42,013 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 29,473 [2] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 53601.

Remove ads

Historia ya Rujewa

Jina Rujewa linatokana na mtu wa kwanza kuishi Rujewa aliyeitwa Mjewa, aliyekuwepo miaka mingi na familia yake wakaitwa Wajewa, ndiyo sababu hata leo hii pakaitwa Rujewa.

Watawala wa jadi

Wenyeji wa mwanzo Rujewa walikuwa Wasangu waliokuwa na mtawala wao wa jadi aliyeitwa Chifu Merere, lakini pia kuna Wabena, Wakinga na hata kuna Waburushi kutoka Pakistan ambao hufanya shughuli kwa kushirikiana na wenyeji.

Uchumi

Rujewa iko katika tambarare ya Usangu ambako maji ya mito kutoka milima ya jirani yanakusanyika na kuwa chanzo cha Mto Ruaha Mdogo. Hivyo eneo linatumiwa kwa kilimo cha umwagiliaji hasa ukiangalia ndiko yaliko mashamba ya Mbarali Estate.

Rujewa ni maarufu hasa kwa kilimo cha mpunga kule Kapunga, ambao unasifika kuwa mzuri kuliko eneo lolote la Tanzania, na baadhi ya mazao ya biashara yanayolimwa Rujewa ni kama alizeti. Pia Rujewa yanastawi mazao mengi ya chakula kama vile karanga, mahindi, ulezi n.k.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads