San Francisco
jiji katika Jimbo la Kaliformia, Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
San Francisco ni mji wa Marekani uliopo kwenye mwambao wa Pasifiki katika jimbo la Kalifornia. Ni mji mkubwa wa nne wa Kalifornia ukiwa na wakazi 744,000.




San Francisco iko kwenye rasi kati ya Pasifiki na hori ya San Francisco. Mlangobahari wa kuingia katika hori huitwa "Golden Gate".
Mji hutembelewa na watalii wengi wanaopenda kuangalia daraja la Golden Gate, kisiwa cha Alcatraz na gereza lake, halafu kuzunguka mjini kwa reli za nyaya.
Mji unajulikana pia kwa jumuiya kubwa za mashoga na wabasha.
Remove ads
Historia
Mji ulianzishwa na Wafransisko Wahispania mnamo 1776 kama sehemu ya koloni lao la Meksiko. Jina limechaguliwa kwa heshima ya mwanzilishi wao, Mt. Fransisko wa Asizi.
Baada ya vita vya Marekani dhidi ya Meksiko ya 1846 mji ukawa sehemu ya Marekani. Uchimbaji wa dhahabu ulisababisha ukuzi wa haraka.
Mwaka 1906 San Francisco iliharibiwa na tetemeko la ardhi ikajengwa upya.
Viungo vya nje
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu San Francisco kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads