Saserdosi wa Lyon

From Wikipedia, the free encyclopedia

Saserdosi wa Lyon
Remove ads

Saserdosi wa Lyon (pia: Sardot au Serdot; 487 - 552[1]) alikuwa askofu mkuu wa mji huo, leo nchini Ufaransa [2][3] kuanzia mwaka 544 hadi kifo chake[4][5].

Thumb
Sanamu ya Mt. Saserdosi katika kanisa la Mt. Paulo, Lyon.

Alikuwa mtoto wa askofu Rustiko wa Lyon ambaye anaheshimiwa kama mtakatifu. Mwenyewe naye, kabla ya kupata uaskofu, aliwahi kuoa na kuzaa mtoto mmoja, Aureliano wa Arles, ambaye pia anaheshimika hivyo [6].

Aliishi daima katika upendo na uchaji wa Mungu akafariki Paris alipokwenda ili kushiriki mtaguso[7].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Septemba[8].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads