Shamu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Shamu (kutokana na Kiarabu ٱلشَّام ash-Shām, inayomaanisha "[nchi] ya kaskazini") ni jina la eneo la kihistoria katika Mashariki ya Kati inayokaliwa leo hii na nchi za Syria, Lebanon, Palestina, Israeli na Yordani. Shamu, iliyojulikana kwa Waarabu kama Bilād al-Shām (بِلَاد الشَّام), ilikuwa mojawapo ya mikoa ya khalifa za Kiumaya, Kiabasi, na Kifatimi.[1]

Mipaka ya kijiografia ilikuwa mto Frati na milima ya Anatolia upande wa kaskazini, Bahari ya Mediteranea upande wa magharibi, Misri upande wa kusini na jangwa la Uarabuni upande wa mashariki.

Ni pia jina la kienyeji la mji wa Dameski linalotumiwa mara nyingi nchini Syria.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads