Simplisiani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Simplisiani
Remove ads

Simplisiani wa Milano (Brivio, Lombardia, Italia, 320 hivi - Milano, 401) alikuwa Askofu wa mji huo tangu mwaka 397 hadi kifo chake.

Thumb
Mt. Simplisiani wa Milano

Alichaguliwa na Ambrosi wa Milano kuwa mwandamizi wake. Augustino wa Hippo alimsifu pia[1][2]. Ni kwamba Simplisiani alipokuwa padri aliwasaidia wote wawili kujiandaa kwa ubatizo kama alivyofanya kwa mwanafalsafa Viktorino.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Agosti[3] ila Milano ni 14 Agosti.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads