Songosongo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Songosongomap
Remove ads

8°31′17″S 39°30′44″E


Thumb
Pwani ya kisiwa cha Songosongo.

Songosongo ni kata ya Wilaya ya Kilwa katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Kata hii inafanywa na kijiji kimoja tu kilichopo kwenye kisiwa cha Songosongo kinachopatikana takriban kilomita 26 kutoka Kilwa Kivinje upande wa kaskazini mashariki kwenye Bahari Hindi.

Remove ads

Wakazi

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,600 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,026 [2] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 65420.

Uchumi

Songsongo ni nyumbani kwa jumuiya ya wavuvi. Kutokana na kukosa soko la samaki na uhaba wa vifaa vya kazi, wengi ni maskini; mnamo 2008 mapato ya wastani yalikuwa TSh 480,000 (wakati ule dollar 330 hivi) pekee kwa mwaka. [3]. Wenyeji wachache walipata ajira kwenye mradi wa gesi.

Mradi wa gesi

Mwaka 1974 gesi asilia iligunduliwa na kampuni ya AGIP kwenye kisiwa cha Songosongo na pia chini ya bahari karibu na kisiwa. Kwa miaka kadhaa ugunduzi haukufuatiliwa kwa sababu ya kukosa soko kwa matumizi yake.

Tangu mwaka 1995 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania pamoja na kampuni ya Globeleq (inayomilikiwa na taasisi za serikali za Uingereza na Norwei) zilianzisha kampuni mpya ya Songas. Songas ilijenga bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam kwa uzalishaji wa umeme[4]. Baada ya kukamilisha bomba, gesi ilianza kufika Dar mwaka 2004 inapotumiwa kwenye kituo cha umeme cha Ubungo.

Kwa mahitaji ya wilaya ya Kilwa ambayo haikuunganishwa bado na mtandao wa umeme wa kitaifa kituo kidogo cha umeme kilijengwa kwenye kata ya Somanga, Kilwa ambako umeme unatengenezwa kwa kutumia gesi kutoka bomba linalofika hapa barani kutoka kisiwa.

Baada ya kupatikana kwa gesi ya Songosongo maeneo ya ziada yalitambuliwa yenye gesi chini ya bahari.[5]

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads