Teodosi abati
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Teodosi abati (Mogarissos, Kapadokia, leo nchini Uturuki, 423 hivi – Yerusalemu, Israeli, 529), rafiki wa abati Saba, alikuwa mmonaki aliyeanzisha na kuratibu maisha ya kijumuia katika monasteri kadhaa huko Palestina. Kabla ya hapo aliiishi muda mrefu kama mkaapweke[1].


Pia alishika sana imani sahihi ilivyofundishwa na Mtaguso wa Kalsedonia na kwa ajili hiyo aliwahi kudhulumiwa sana na serikali ya Dola la Roma Mashariki.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Januari.[2][3]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads