Teofilo wa Corte

From Wikipedia, the free encyclopedia

Teofilo wa Corte
Remove ads

Teofilo wa Corte (Corte, Corsica, leo nchini Ufaransa, 30 Oktoba 1676 - Fucecchio, leo nchini Italia, 19 Mei 1740), mwanafunzi wa Thomas wa Cori, alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo na mhubiri maarufu.

Thumb
Sanamu yake katika kanisa la Alando.

Jina lake la awali lilikuwa Biagio Arrighi. Alijulikana kwa heshima yake kubwa kwa Mateso ya Yesu na kwa Bikira Maria.

Alijitahidi kueneza urekebisho shirikani kwa kuanzisha mahali pa upwekeni[1].

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu tarehe 29 Juni 1930, alipotangazwa na Papa Pius XI.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads