Teolojia ya shule

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Teolojia ya shule (kwa Kilatini: Theologia Scholastica) ni aina ya teolojia iliyoanza katika shule za monasteri zilipogundua upya falsafa ya Aristoteli kupitia tafsiri za wanafalsafa Wayahudi na Waislamu.

Katika juhudi ya kulinganisha metafizikia hiyo na teolojia ya Ukristo wa Magharibi, iliwekwa misingi ya vyuo vikuu vya Karne za Kati, na hatimaye ya ustawi wa sayansi.

Teolojia hiyo ilitawala elimu ya Ulaya miaka 1100-1700 hivi[1].

Kati ya wawakilishi wakuu wa shule hiyo kuna: Anselm wa Canterbury ("baba wa falsafa ya shule"[2]), Petro Abelardo, Aleksanda wa Hales, Alberto Mkuu, Yohane Duns Scotus, William wa Ockham, Bonaventura wa Bagnoregio, na Thoma wa Akwino. Kitabu chake bora, Summa Theologica (12651274) kinahesabika kilele cha falsafa ya shule, ya Karne za Kati na ya Kikristo kwa jumla[3].

Remove ads

Tanbihi

Vyanzo vikuu

Vyanzo vingine

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads