Theobadi wa Provins
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Theobadi wa Provins, O.S.B. Cam. (kwa Kifaransa: Thibaud; 1033 – 30 Juni 1066) alikuwa mtoto wa mtawala wa Champagne, Ufaransa[1], aliyevutiwa sana na maisha ya Yohane Mbatizaji na ya Mababu wa jangwani[2], hivyo akaenda kujiunga na monasteri huko Reims.

Baadaye, akiongozana na rafiki Walter, aliishi kama mkaapweke katika mahali na nchi mbalimbali ili kukwepa watu waliowatafuta ili kuwaheshimu[3].
Kabla hajafa alipewa upadrisho ili kuongoza vizuri zaidi wanafunzi alioanza kupokea akajiunga na Wabenedikto Wakamaldoli huko Sassano, Italia[4].
Papa Aleksanda II alimtangaza mtakatifu mwaka 1073.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads