Thoma Hioji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Thoma Hioji, O.P. (Hirado, 1590 - Nagasaki, 17 Novemba 1634) alikuwa padri kutoka Japani na mmojawapo kati ya Wakristo wa Kanisa Katoliki waliofia dini nchini humo.

Katikati alifanya umisionari huko Taiwan[1].
Aliuawa kwa kunyongwa ameng'inginizwa juu ya shimo la jalala pamoja na padri Mdominiko mwenzake Jordano Ansalone [2] kwa amri ya amirijeshi Tokugawa Yemitsu baada ya kuvumilia siku saba za kuteswa.
Anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na Lorenzo Ruiz na wenzao waliotangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa wenye heri tarehe 18 Februari 1981 halafu watakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads