Jordano Ansalone

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jordano Ansalone
Remove ads

Giacinto Giordano Ansalone, O.P. (Santo Stefano Quisquina, Sicilia, 1598 Nagasaki, 17 Novemba 1634) alikuwa padri mmisionari kutoka Italia na mmojawapo kati ya Wakristo wa Kanisa Katoliki waliofia dini nchini Japani.

Thumb
Mt. Jordano alivyochorwa.
Thumb
Mchoro wa Kijapani ukiwaonyesha Wafiadini wa Nagasaki, karne ya 16 na ya 17.

Kabla ya kutumwa huko aliinjilisha kwa ari Ufilipino.

Aliuawa kwa kunyongwa ameng'inginizwa juu ya shimo la jalala pamoja na padri Mdominiko mwenzake Thoma Hioji kwa amri ya amirijeshi Tokugawa Yemitsu baada ya kuvumilia siku saba za kuteswa kikatili[1].

Anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na Lorenzo Ruiz na wenzao waliotangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa wenye heri tarehe 18 Februari 1981 halafu watakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads