Lorenzo Ruiz
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Lorenzo Ruiz (kwa Kichina: 李樂倫; Binondo, Manila, Ufilipino 1600 hivi – Nagasaki, Japani 29 Septemba 1637),[1] ni Mfilipino[2] wa kwanza kutangazwa mtakatifu na Kanisa Katoliki[3].

Mlei huyo alifia dini ya Ukristo kisha kukataa kuhama Japani na kukana imani yake wakati wa dhuluma za watawala wa Edo (leo Tokyo) kutoka ukoo wa Tokugawa katika karne ya 17.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mfiadini mwenye heri tarehe 18 Februari 1981, halafu mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.
Pamoja naye walitangazwa watakatifu na wanaheshimiwa kama wafiadini wa Japani (1633–1637):[4][5][6]
- Antonio Gonzalez
- Dominiko Ibáñez de Erquicia
- Yakobo Kyushei Tomonaga
- Fransisko Shoyemon
- Jordano Ansalone
- Lazaro wa Kyoto
- Luka Alonso
- Marina wa Omura
- Magdalena wa Nagasaki
- Mathayo Kohioye
- Mikaeli wa Aozaraza
- Mikaeli Kurobioye
- Thomas Rokuzayemon
- Vinsenti Shiwozuka
- William Courtet
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba[7].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads