Tipasi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tipasi (kwa Kilatini: Typasius; alifariki 10 Januari 297 au 298[1]) alikuwa askari kutoka Tigava (leo El Kherba, nchini Algeria).
Baada ya kuingia Ukristo na kuacha maisha ya jeshi, alipoitwa na kaisari Maksimiani kusaidia katika vita dhidi ya wenyeji Quinquegentiani waliotaka kupinga mamlaka ya Dola la Roma, Tipasi alikataa[2].
Baadaye alianzisha monasteri alipoishi muda mrefu. Hatimaye aliitwa tena jeshini na kudaiwa kutoa sadaka kwa miungu ya Roma. Hapo akakatwa kichwa.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Januari[3][4].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads