Tukiko
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Tukiko alikuwa Mkristo wa karne ya 1 kutoka mkoa wa Asia ambaye alimfuata Mtume Paulo katika baadhi ya safari zake, na ambaye anatajwa kwa sifa katika vitabu vitano vya Agano Jipya (Mdo 20:4; Ef 6:21-22; Kol 4:7; Tito 3:12; 2 Tim 4:12). Paulo mwenyewe anamuita "Ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu na mwenzi katika huduma ya Bwana"[1][2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads