Chuo Kikuu cha California, Los Angeles
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Chuo Kikuu cha California, Los Angeles, au kwa kifupi UCLA, ni chuo kikuu kilichopo Los Angeles, California. Kilianzishwa mwaka 1919. Mara nyingi huorodheshwa miongoni mwa vyuo bora zaidi Marekani.


Chuo hicho kilianza kama chuo cha walimu, lakini kikawa chuo kikuu mwaka hu huo wa 1919, kikaanza kuitwa UCLA mwaka 1927. Hapo awali kilikuwa Hollywood, lakini sasa kiko Westwood. Mwaka 1950, kilijitenga rasmi kutoka University of California, Berkeley. Katika miaka ya 1960 na 1970, wanafunzi wengi walifanya maandamano.[1]
Chuo kina majengo yaliyobuniwa na mbunifu wa majengo maarufu, bustani nyingi, chemchemi na makumbusho. Kina programu za masomo mbalimbali, ikiwemo Shule maarufu ya filamu na kozi za tiba zinazoshirikiana na hospitali kadhaa. Chuo kimegawanywa katika kozi za taaluma 12 zinazotoa digrii kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza na ya juu. Kozi hizo ni: Sayansi na Sanaa, Sanaa na Usanifu, Uhandisi, Muziki, Uuguzi, Masuala ya Umma, Sanaa ya Maonyesho, Filamu na Televisheni, Tiba, Udaktari wa Meno, Afya ya Umma, Elimu na Masomo ya Habari, Usimamizi na Sheria.
UCLA ina timu nyingi nzuri za michezo zinazoshiriki katika mashindano ya kiwango cha Division I. Timu zao, ambazo hushindana katika Big Ten Conference[2] na Pacific-12 Conference, huitwa Bruins, yaani "dubu wadogo." Timu hizi zimeshinda ubingwa 103. Timu ya mpira wa vikapu hucheza kwenye ukumbi wa Pauley Pavilion na imeshinda mataji 11, ikiwa na wachezaji maarufu kama Kareem Abdul-Jabbar, Bill Walton, na Gail Goodrich. Wachezaji wa sasa wa NBA kama Kevin Love, Russell Westbrook, na Lonzo Ball pia waliwahi kuichezea timu ya wanaume ya mpira wa vikapu ya UCLA. Timu ya mpira wa miguu hucheza kwenye uwanja wa Rose Bowl, ambao pia hutumika kwa mchezo maarufu wa bowl kwa jina hilo. UCLA pia ina timu nzuri za voliboli na polo ya maji, na imepeleka mamia ya wanamichezo kwenye Michezo ya Olimpiki. UCLA ina ushindani mkubwa wa michezo dhidi ya USC, chuo kingine kikuu kilichopo Los Angeles. Pia kuna ushindani mdogo na Stanford, Cal na Notre Dame.
Remove ads
Wahitimu maarufu
- Kareem Abdul-Jabbar (1969), mchezaji wa zamani wa NBA
- Nicolas Sadirac (1986), mwanzilishi wa École pour l'informatique et les nouvelles technologies[3]
- Jack Black (1989), mwigizaji, mchekeshaji, na mwanamuziki
- Randall Park (1997), mwigizaji, mwandishi wa filamu, na mtayarishaji
- Ben Shapiro (2004), wakili, mwandishi wa makala, na mchambuzi wa siasa za kihafidhina
- Mayim Bialik (2007), mwigizaji, mtaalamu wa neva, mwandishi na mtangazaji wa zamani wa kipindi cha michezo
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads