Ufunguo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ufunguo
Remove ads

Ufunguo (kutoka kitenzi "kufunga", kinyume chake "kufungua") ni kifaa kinachotumika kufungulia au kufungia mlango, kufuli n.k.

Thumb
Ufunguo wa Waviking wa Uingereza (900 hivi BK)
Thumb
Kufuli za karne za kati huko Kathmandu (Nepal).

Kwa sababu hiyo, mara nyingi huchukuliwa kama ishara ya kumiliki nyumba, sanduku n.k. Mwambatanisho wa kufuli na ufunguo huchangia katika ulinzi kwa maana ni mwenye ufunguo peke yake anayeweza kufungua kitasa au kufuli.

Remove ads

Historia ya ufunguo

Historia ya ufunguo inafanana na ile ya kufuli maana zote zilitengenezwa kwa pamoja. Kufuli na ufunguo wa kwanza zilipatikana kule Ninawi, Assyria.[1] Baadaye, mwambatanisho huo ulipatikana nchini Misri.[2]

Baada ya mfumo huu wa ulinzi kuitikiwa na wote, uvumbuzi uliendelezwa na teknolojia pia kutumika katika kuboresha kufuli na funguo.

Leo, funguo za kisasa zahitilafiana sana na zile za zamani. Hata hivyo, minajili ni ilele: ulinzi.

Remove ads

Funguo za kisasa

Thumb
Ufunguo wa kawaida wa kisasa.

Funguo za leo zina ulinzi mwingi kuliko ule wa zamani. Wezi waliweza kufungua na kuingia kwenye nyumba za kufuli za kitambo maana zilitengenezwa kwa teknolojia dhaifu.

Hivi leo, teknolojia ni nzuri na ni vigumu (hata kama bado itafanyika) kufungua kufuli kwa ufunguo usiodhaminiwa kufanya hivyo. Pia kuna teknolojia ambayo inazuia mtu kutengeneza nakala ya ufunguo bila ruhusa ya mwenye ufunguo.

Pia kumekuwa na kufuli zisizohitaji ufunguo wa kawaida bali tu kubofya nambari. Milango hii ni kama ile ya karakana za gari, ya milango ya nyumba na kampuni.

Kuna milango pia ambayo hufunguliwa kwa njia ya kieletroniki baada ya kutambua anayejaribu kufungua.

Remove ads

Funguo na taaluma ya lokismithi

Upotevu wa funguo au kuvunjika kwa funguo hufanya mtu ateseke sana akijaribu kuufungua au hata kuuvunja mlango. Kwa kuepuka hii shida, watu wengi huona heri waende kwa walio na taaluma ya lokismithiambayo ni taaluma ya kutengeneza funguo, kufuli na usalama wote wa kinyumbani. Lokismithi hawa huweza kuifungua ile milango kwa kutengeneza funguo badala au kuikata kufuli.

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads