Ninawi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ninawi (kwa Kiakadi: Ninwe; kwa Kiashuru: ܢܸܢܘܵܐ; kwa Kiebrania נינוה , Nīnewē; kwa Kigiriki Νινευη, Nineuē; kwa Kiarabu: نينوى, Naīnuwa) ulikuwa mji mkuu wa Waashuru upande wa mashariki wa mto Tigri.
Magofu yake yako ng'ambo ya mto huo ukitokea Mosul (Iraki).
Mji huu ulikuwa mkubwa kuliko yote duniani[1] kwa miaka hamsini hadi mwaka 612 KK uliposhindwa na Wababuloni.[2]
Katika Biblia ni maarufu hasa kutokana na habari zinazopatikana katika kitabu cha Yona na zilizotumiwa na Yesu kuhimiza toba akisema watu wa Ninawi watasimama kuhukumu watu ambao hawatatubu siku za mwisho[3] .
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads