Ustaarabu wa magharibi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ustaarabu wa magharibi
Remove ads

Ustaarabu wa magharibi ni utamaduni wenye taratibu za kijamii, maadili, desturi, sheria, falsafa, imani, siasa, sanaa na teknolojia maalumu ambavyo asili yake ni Ulaya hata kame vimezidi kustawi sehemu nyingine za dunia ambazo historia yake ilikuwa na uhusiano wa pekee na bara hilo.

Thumb
Plato, ambaye pamoja na Sokrates na Aristotle, aliweka msingi wa falsafa ya magharibi.
Thumb
Mchoro maarufu wa Leonardo da Vinci unaoonyesha umuhimu wa binadamu katika mtazamo wa magharibi kuanzia Renaissance.
Thumb
The Beatles, bendi lililouza albamu nyingi kuliko yote, linaendelea kuathiri magharibi si upande wa muziki tu.
Thumb
Aina kuu za ustarabu baada ya mwaka 1990 kadiri ya Huntington (ule wa magharibi una rangi ya buluu iliyokolea).

Kwa kiasi kikubwa ni urithi wa Ugiriki wa Kale, Roma wa Kale, Uyahudi,[1] na utamaduni wa makabila mengine[2][3]lakini hasa wa Ukristo na madhehebu yake ya kwanza, Kanisa Katoliki,[4][5][6][7][8][9][10][11] pamoja na Makanisa ya Kiorthodoksi[12][13].

Baada ya Matengenezo ya Kiprotestanti, athari yake imekuwa kubwa pia, hasa Ulaya Kaskazini na makoloni yake, kama yale yaliyounda Marekani, ambayo katika karne ya 20 imeshika uongozi wa dunia na kuzidi kusambaza ustarabu huo.[14][15]

Tabia yake ya msingi ni kujali na kustawisha akili badala ya kutegemea visasili na mapokeo. Ilikuwa hivyo kuanzia falsafa ya Shule ya Athene, ikaendelea baada ya uenezi wa Ukristo kupitia Teolojia ya Shule, Renaissance, Mapinduzi ya Kisayansi hadi Falsafa ya Mwangaza. Hiyo ilisaidia kutambua tunu kama haki za binadamu, usawa na demokrasia. [16]

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads