Visensya Gerosa

From Wikipedia, the free encyclopedia

Visensya Gerosa
Remove ads

Visensya Gerosa (kwa Kiitalia Vincenza Gerosa; (29 Oktoba 178420 Juni 1847) alikuwa mwanamke wa Italia kaskazini ambaye, pamoja na Bartolomea Capitanio, alianzisha shirika la Masista wa Upendo wa Lovere, ambao kwa kawaida wanaitwa Masista wa mtoto Maria[1].

Thumb
Visensya Gerosa akifanya utume wake.

Maisha

Visensya alizaliwa katika kijiji cha Lovere, mkoani Lombardia, katika familia tajiri. Jina lake la awali lilikuwa Caterina.

Alikutana na Bartolomea alipokuwa na umri wa miaka 40, wakaungana kupambana na ujinga na ufukara wa watu wa eneo lao.

Baada ya Bartolomea kufariki, Visensya aliendeleza shirika lao kwa miaka mingi akafariki mwaka 1847 hukohuko Lovere.

Wote wawili walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 30 Mei 1926, halafu watakatifu na Papa Pius XII tarehe 18 Mei 1950.

Sikukuu ya Visensya inaadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Juni[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads