Waaramu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waaramu (ܐܪ̈ܡܝܐ, ʼaramáyé), ni watu wa jamii ya Wasemiti wa kaskazini[1] ambao wanatumia Kiaramu.


Mwishoni mwa kipindi cha shaba (karne ya 11 hadi karne ya 8 KK) waliunda shirikisho la makabila kutoka Syria ya leo.
Bila kuungana kabisa, walianzisha falme kadhaa kote katika Mashariki ya Kati na kuteka sehemu kubwa ya Mesopotamia.
Katika karne nne za kwanza BK walipokea Ukristo kwa namna maalumu yaliyojitokeza hasa katika shemasi Efrem Mshamu.
Baada ya maeneo yao kutekwa na Waarabu Waislamu (karne ya 7) walizidiwa na kupotewa taratibu na lugha na desturi zao. Hata hivyo baadhi wapo hadi leo[2][3][4]
Remove ads
Tanbihi
Vyanzo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads