Waaugustino
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Waaugustino ni hasa watawa wanaofuata kanuni ya Agostino wa Hippo. Kwa Kilatini shirika lao linaitwa Ordo Fratrum Sancti Augustini. Tangu muda mrefu linahesabiwa kati ya mashirika ya ombaomba.
Historia
Katika karne XII zilikuwepo jumuia nyingi zilizofuata kanuni hiyo. Katikati ya karne XIII, kwa juhudi za kardinali Riccardo Annibaldi, ulianza mchakato wa kuziunganisha.
Tarehe 16 Desemba 1243 Papa Inosenti IV alitoa hati Incumbit nobis ili kuhimiza mchakato huo, hata Machi 1244 shirika likaanzishwa.
Baadhi ya Waaugustino katika karne zilizofuata walifanya juhudi za urekebisho na kuanzisha matawi mapya.
Remove ads
Takwimu
Mwaka 2025, mbali na matawi hayo yaliyojitegemea, shirika lilikuwepo katika mabara yote likiwa na konventi 395 na watawa 2,341, wengi kati yao walikuwa mapadri.[1] Maarufu zaidi kati yao ni Papa Leo XIV, Papa wa kwanza kutoka shirika hilo.
Kati ya nchi 46 ambako shirika linaishi, kuna Kenya na Tanzania.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads