Xi'an
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Xi'an ni makao makuu ya Mkoa wa Shaanxi nchini China. Kwenye mwaka 2011 ilikuwa na wakazi milioni 6. [2]

Jiji hilo ni maarufu kwa Jeshi la Matofali lililopatikana ndani ya kaburi la kaisari wa kwanza wa China Qin Shi Huang. [3]
Remove ads
Historia
Mji huu ulikuwa mji mkuu wa nasaba za wafalme 13, pamoja na nasaba ya Zhou, nasaba ya Qin, nasaba ya Han, nasaba ya Sui, na nasaba ya Tang.
Umuhimu wa mji ulitokana na mahali pake kwenye chanzo cha Barabara ya Hariri iliyounganisha China na Asia ya Magharibi na ya Kusini [4].
Xi'an inachukuliwa kuwa moja ya taji za kongwe zaidi katika historia ya ulimwengu pamoja na nyingine tatu za Athene, Roma na Cairo.
Remove ads
Jina
Xi'an ilijulikana zaidi kwa tahajia ya Sian. Jina la Xi'an lilichaguliwa kwa maana ya "Amani ya Magharibi" wakati wa nasaba ya Ming kwa sababu ilikuwa mji mkubwa kwenye magharibi ya milki ya Ming.
Utamaduni na Utalii
Kama mji wa kihistoria, Xi'an bado imezungukwa na ukuta wa kale. Kivutio kikuu cha wageni ni makaburi ya kifalme pamoja na "jeshi la matofali". Halafu:
- Banpo: kijiji cha zama za mawe
- Ukuta wa mji
- Mnara wa kengele na ngoma
- Pagoda wa bata bukini mwitu
- Kaburi la Hanyangling
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads